






























Mshambuliaji mpya wa Klabu ya Simba, Jonathan Sowah, ataikosa mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga itakayopigwa Septemba 16, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.
Hii ni baada ya kufungiwa kufuatia kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB msimu uliopita wakati akiwa na Singida Black Stars.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu Tanzania Bara, mchezaji anapopata kadi nyekundu katika michezo ya FA anatakiwa kutumikia adhabu hiyo kwenye mechi zinazofuata za mashindano ya ndani, ikiwemo Ligi Kuu Bara, na pia Ngao ya Jamii.
Hii inamaanisha kwamba Sowah hataruhusiwa kushiriki mchezo huo wa ufunguzi wa msimu mpya.
0 Comments:
Post a Comment