Maandalizi ya uwanja tayali kwa ajili ya Simba na Mtibwa kesho
Mapema leo maafisa wa Chama cha Soka mkoani Maorogoro walisimamia ufyekwaji wa nyasi kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Simba.
Mchezo huo utapigwa kesho Jumatatu, April 09 2018.
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika.
"Tunakwenda kucheza na moja ya timu bora VPL..lakini inabidi tupate matokeo chanya ili tutimize lengo," amesema Manara
"Timu ipo tayari kwa mchezo huu..ombi langu ni lile lile, .msiache kutuombea."
0 Comments:
Post a Comment