Thursday, 7 June 2018

Uhai Cup mechi zote kupigwa Dodoma

TIMU ya Simba Sc, Azam Fc, Yanga Sc na Tanzania Prisons wameibuka viongozi wa makundi yaliyopatikana katika Droo ya michuano ya vijana chini ya miaka 20 iliyochezeshwa leo makao makuu ya Azam Tv.

Mechi zote zimepangwa kuanza Juni 9 hadi 21 zitapigwa Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambapo timu  12 zitashiriki.

Kundi A litaongozwa na Yanga Africans Ruvu Shooting, Mbeya City, na Mbao FC huku Kundi B kiongozwa na Simba, Singida United, Stand United na Njombe Mji.

Kundi C linaongozwa na Azam, Mtibwa Sugar, Mwadui FC na Majimaji FC huku Kundi Dlikiongozwa na Tanzania Prisons, Lipuli FC, Kagera Sugar na Ndanda FC.

0 Comments:

Post a Comment