Wednesday, 6 June 2018

Yaya Toure afunguka haya akisema Guardiola ni mtu mbaguzi na mwenye wivu

KIUNGO wa Ivory Coast, Yaya Toure ambaye ameachana na timu ya Manchester City mwishoni mwa msimu uliomalizika, hivi karibuni amesema kocha wa timu hiyo, Pep Guardiola, ni mtu mbaguzi na mwenye wivu.

Yaya alibainisha hayo juzi, huku akisisitiza Guardiola hawapendi wachezaji kutoka Bara la Afrika.

Kiungo huyo alifanya kazi na Guradiola kwa miaka miwili wakati yupo Barcelona kabla hajauzwa kwenda Manchester City mwaka 2010 kwa ada ya pauni milioni 24.

“Guardiola hana mahusiano mazuri na wachezaji kutoka Afrika, namfahamu tangu nilipokuwa naye Barcelona.

“Mara nyingi huwa na wivu, lakini anakuchukia bila sababu yoyote, amekuwa hivyo mara zote,” alisema Yaya.

Msimu uliomalizika hivi karibuni Yaya alifanikiwa kuanza mchezo wa mwisho dhidi ya Brighton na kutoka dakika ya 86.

0 Comments:

Post a Comment