Saturday 21 July 2018

Asseums afunguka kilichomleta Simba

Mbelgiji Patrick Asseums  alisaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo, Asseums amesema alikuwa na ofa nyingi kutoka timu za Afrika, lakini aliona Simba kunaweza kuwa sehemu muafaka baada ya kufanya mazungumzo na Mwekezaji wa klabu hiyo, Mohamed Dewji (MO).

"Ndio, nimeamua kuja hapa baada ya kuzungumza na Dewji kwa kina na akanieleza mipango yake kuwa anataka Simba kuwa klabu kubwa Afrika. Nina uzoefu wa kutosha hivyo, nauleta hapa kwa ajili ya kutimiza malengo hayo,” alisema.

Patrick aliongeza kuwa anafahamu Simba ni klabu kubwa nchini lakini, dhamira yake ni kuifanya kuwa tishio barani Afrika.

“Najua Simba hapa iko juu, ila lengo langu ni kuhakikisha inaendelea kuwa juu Afrika, watu wazidi kuielewa,” alisema.

Kocha huyo ameweka bayana kwamba hataki soka la Kiingereza la pasi mbili wako golini wanafunga na kama wachezaji watashindwa kwenda na staili hiyo basi watapata tabu sana.

“Kila mwalimu ana falsafa yake ya ufundishaji, timu yangu nataka imiliki mpira na kucheza soka la utulivu, sitaki wanapiga pasi mbili wako golini kwa wapinzani wanafunga bao, hapana hiyo staili yangu kabisa,” alisema.

Pia, alifichua kuwa anapenda kuwa kwenye timu ambayo wachezaji wake wanakuwa na furaha uwanjani kwa kuwa itasaidia kuwapa morali.

0 Comments:

Post a Comment