Friday, 13 July 2018

Azam FC yafanikiwa kutetea Ubingwa wake Kagame Cup

Azam FC imefanikiwa kutetea ubingwa wa kombe la Kagame baada ya kuilaza Simba mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Mabao ya Azam FC yalifungwa na Shabani Iddi Chilunda na Aggrey Morris wakati bao pekee la Simba liliwekwa kambani na Meddie Kagere.

Azam FC pia ilikosa mkwaju wa penati kupitia mlinda lango wake Razak Abalora.

Azam FC ilikuwa timu ya mwisho kuchukua taji hilo mwaka 2015, michuano hiyo haikufanyika kwa miaka mitatu kabla ya mwaka huu ambapo Azam Fc imetwaa tena taji hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Gor Mahia iliilaza JKU mabao 2-0.

Azam FC imejinyakulia kitita cha dola 30,000 wakati Simba imefanikiwa kuondoka na dola 20,000 na Gor Mahia ikiondoka dola 10,000

Mshambuliaji wa Azam FC Shabani Iddi Chilunda ameibuka kuwa mfungaji bora wa michuano baada ya kufunga mabao nane akifuatiwa na Meddie Kagere wa Simba aliyefunga mabao manne.

Chilunda tayari amesajiliwa na klabu ya Tenerife inayoshiriki ligi daraja pili (Segunda B) ya nchini Hispania.

0 Comments:

Post a Comment