Wednesday, 11 July 2018

England yatolewa kombe la Dunia

Mojawapo ya mbwembwe za mashabiki wapatao 7, 000 wa Uingereza waliomiminika jijini Moscow, wengine wakiwa wamevalia visibao kama kocha wao  Gareth Southgate  zimezimika  usiku huu ambapo badala ya kurudisha mwali nyumbani inabidi warudi labda na ushindi wa tatu. 

Croatia usiku huu imekuwa nchi 'tofauti' ya 13th kutinga fainali ya Kombe la Dunia la soka na ya 10 kutoka Ulaya kwa kuipiga Uingereza goli 2-1 katika dakika 120 baada ya kufungana 1-1 katika dakika 90 za kawaida. Shujaa wa Croatia yenye watu milioni 4 alikuwa ni huyo  Mario Mandzukic aliyetia kimiani bao katika dakika ya 11 kabla ya filimbi ya mwisho kwa pasi tamu ya kichwa toka kwa Ivan Perisic.

0 Comments:

Post a Comment