Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kushuka dimbani leo kukipiga dhidi ya Gor Mahia FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Mkongomani, Mwinyi Zahera, amesema watahakikisha wanaimaliza timu hiyo.
Zahera ambaye amechukua mikoba ya Mzambia George Lwandamina, amesema watatumia udhaifu wa Gor Mahia waliouonesha katika mashindano ya KAGAME yaliyomalizika wiki jana jijini Dar es Salaam.
Kocha huyo ameeleza kuwa Gor Mahia wana timu ambayo imekaa muda mrefu lakini mapungufu yao yapo katika safu ya ulinzi, hivyo watatumia mwanya huo kupata matokeo.
Zahera amesema wapinzani wao wapo vizuri ila kupitia nafasi ya ulinzi bado ina shida kidogo kwao na amaanini wanaweza kuitumia ili kupata matokeo chanya
Ikumbukwe Yanga haijapata ushindi wowote tangu kuangukia mashindano ya Kombe la Shirikisho baada ya kuondoshwa Ligi ya Mabingwa Afrika na kesho watajituma kuhakikisha wanapata matokeo.
Yanga imeenda suluhu pekee ya 0-0 dhidi ya rayon Sports ya Rwanda huku ikipoteza mchezo mmoja dhidi ya MC Algeria ya Algeria kwa kufungwa mabao 4-0 ugenini.
0 Comments:
Post a Comment