Ofisa Habari wa klabu ya Simba amezungumzia kichapo walichokipata watani zao wa jadi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia FC cha mabao 4-0.
Manara ambaye amekuwa akiwatania Yanga haswa kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii mara nyingi, amewapa pole akisema kuwa ni sehemu ya mchezo.
Mbali na pole hizo, Manara ameeleza kuwa wakati akihamasisha timu hizo zipeane uzalendo wakati Simba alipokuwa anajiandaa kushiriki mashindano ya Shirikisho Afrika, amesema Yanga walikataa ombi lake.
Manara amesema kitendo cha Yanga kupingana naye kilimfanya Manara kuendelea kuiombea mabaya Yanga na kipigo cha jana amekielezea kama faraja kwake huku akiwapa pole ya kiaina.
Yanga walikubali idaidi hiyo ya mabao juzi Jumatano huko Nairobi, Kenya na kujiwekea mazingira magumu ya kuendelea kusalia kunako mashindano hayo wakiwa wana alama moja pekee katika kundi D.
MC Alger ipo kileleni ikiwa na alama moja wakifuatia na Gor Mahia wenye alama 5 huku Rayon Sports ya Rwanda ikiwa na mbili na Yanga wakiwa na moja pekee.
0 Comments:
Post a Comment