Monday, 16 July 2018

Mapokezi ya Ufaransa baada kutwaa kombe la dunia

Baada ya kusubiri kwa takiribani miaka 20 hatimaye hii leo kwa mara ya pili wananchi wa Ufaransa wamepata kuliona kombe la dunia likipita nchini mwao baada ya Ufaransa kushinda kombe hilo nchini Urusi, hapa nia matukio ya namna Ufaransa ilivyokuwa hii leo.

Hapa ni wakati wachezaji wanashuka kwenye ndege, tayari kupita na kombe mitaa ya Paris kwa ajili ya wananchi kuliona kombe.

Paul Pogba akishuka kwenye ndege na kuusalimia umati uliokuja kuwapokea uwanja wa ndege.

Hii ni Paris ambapo maelfu ya mashabiki walijipanga pembezoni mwa bara bara wakishangilia mashujaa wao.

Ulinzi nao asikuambie mtu, askari walizunguka basi la wachezaji huku na huku kuhakikisha hakiharibiki kitu.

Hugo Lloris ambaye pia ni nahodha wa timu ya taifa akishuka na kombr kwenye ndege na hapo chini akifurahia kombe pamoja na raisi Emmanuel Macron.

Blue, nyeupe na nyekundu rangi ya bendera ya Ufaransa ilitawala hii leo na fataki zilipigwa zikitoa rangi hiyo.

Mji mzima wa Paris leo kulikuwa hakuna kazi na wananchi waliungana barabarani kushuhudia zawadi kubwa zaidi katika soka Ulimwenguni ikipita nchini kwao.

0 Comments:

Post a Comment