Baada ya kuondokewa na wachezaji wake tegemeo, uongozi wa klabu ya mtibwa Sugar umefunguka na kueleza kuwa sasa watakiboresha upya kikosi chao kwa kuwatumia vijana walionao.
Kupitia Msemaji wa timu hiyo, Thobias Kifaru, amesema kuwa wao ni chuo cha soka hivyo hawana wasiwasi wowote juu ya kuondoka kwa wachezaji wao wawili kuelekea klabu kongwe za Kariakoo.
Kifaru ameeleza Mtibwa itawapasa kuandaa vijana wengine kama ilivyo sera yao ya kuwafua vijana na baadaye wanaimarika kisha kufanua vizuri kama ilivyokuwa kwa Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim na wengineo.
"Tutatumia vijana tulionao kutokana na utamaduni wetu wa kuwafua vijana ambao huwa wanakuja kuwa na vipaji vizuri, kuondoka kwa Dilunga na Banka kwetu wala haitupi shida kubwa" alisema.
Mtibwa imeondokewa na wachezaji Mohammed Issa Banka pamoja na Hassan Dilunga ambao wote wanacheza nafasi ya kiungo.
Banka amefanikiwa kunaswa na Yanga na kusainishwa mkataba wa miaka miwili pia Dilunga akitia kandarasi ya miaka miwili na Simba.
0 Comments:
Post a Comment