Saturday 21 July 2018

Prisons kuweka kambi Sumbawanga

Kikosi cha Prisons ya Mbeya, kitasafiri hadi Sumbawanga kuanza kambi yao kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya.

Kocha Hassan Motego amesema watacheza mechi tatu za kirafiki wakiwa huko.

“Mjini Sumbawanga tutacheza mechi hizo tatu na wenyeji wetu chama cha mpira huko wanajua.

“Baada ya hapo tutarejea Mbeya kabla ya kuendelea na maandalizi mengi kama kwenda Zanzibar,” alisema.

Prisons watakuwa wanawavaa Simba Agosti 22 katika mechi ya Ligi Kuu Bara ikwa ni mechi yao ya kwanza ya ufunguzi wa ligi hiyo.

0 Comments:

Post a Comment