Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ameibuka mshindi wa tuzo ya Afrika katika masuala ya uchumi.
Makamo mwenyekiti wa kamati ya tuzo ya ukombozi Afrika, Mwebesa Rwebugia ameieleza BBC kwamba rais Magufuli ameibuka mshindi kutokana na mchango wake wa kiuchumi hasaa katika ukuaji wa miundo mbinu.
Hii ni mara ya pili kwa kiongozi wa Tanzania kupata tuzo hii, baada ya Mwalimu Julius Nyerere kutuzwa pia kutokana na mchango wake wa kuleta uhuru katika nchi za Afrika.
Mwebesa Rwebugia ameeleza kuwa, katika kuegemea kwenye muktadha wa uchumi, kamati iliangalia umaskini ambao unatajwa kuwa adui mkubwa anayefahamika, lakini pia maradhi na ujinga.
Kwa mujibu wa kamati hiyo ya Tuzo ya Ukombozi wa Afrika, ukombozi katika kipengelee cha elimu huangazia elimu na ujinga kama sehemu ya ukombozi.
Tanzania imetolewa mfano wa elimu ya bila malipo kutoka kutoka shule za msingi mpaka sekondari.
0 Comments:
Post a Comment