Friday, 20 July 2018

Ten akanusha kujiuzulu Yanga

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa amejiuzulu nafasi yake.

Ten ambaye alikuwa nje ya ofisi kwa wiki kadhaa kutokana na kuugua maradhi yaliyosababisha akalazwa, amesema yeye bado ni mwajiriwa wa Yanga.

Baadhi ya magazeti leo yameripoti kuwa Ten amejiuzulu nafasi yake baada ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu, Charles Mkwassa.

Taarifa hizo zimebainisha kuwa Ten amejiondoa Yanga sababu kuu ikielezwa kukosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi wa mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara.

0 Comments:

Post a Comment