Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu Antony Mavunde amewataka vijana kuchangamkia fursa ambazo zinapatikana na kufuatilia taarifa za maendeleo katika halmashauri zao.
Mavunde amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2018/2019 serikali imetenga Bilioni kadhaa kwaajili ya maendeleo ya vijana wa Tanzania na kuwataka kuamka sasa.
“Serikali chini ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu imetenga bilioni kumi na tisa (19) kwa ajili ya mifuko yote inayoshughulikia maendeleo ya vijana, na bilioni moja kwa ajili ya mikopo kwa vijana ambao wamejikita katika ujasiliamali ili kujikomboa kiuchumi”, amesema Mavunde.
kwa mujibu wa mfuko wa maendeleo ya vijana nchini ‘Youth development program( YDP)’ umeweka vigezo vya kupata mikopo hiyo katika halmashauri kuwa vijana wanapaswa kuandaa mpango wa biashara ‘business plan’ na kuunda vikundi na kuwasilisha mawazo hayo katika halmashauri kwa ajili ya kupata mikopo ambapo riba ya mkopo husika hutegemea kiwango na aina ya mkopo.
Aidha Mavunde ameongeza kuwa serikali imeagiza wakurugenzi wa halmashauri zote nchini kutenga asilimia nne ya mapato inayakusanywa katika halmashauri zao kwa ajili ya maendeleo ya vijana kulingana na mabadiliko ya sheria ya fedha ya mwaka 2018/2019.
0 Comments:
Post a Comment