Mashabiki wengi wa Simba wangependa kujua nyota wao, Emmanuel Okwi na nahodha John Bocco wanarejea lini na kuungana na wenzao.
Wakati wowote kuanzia jana, Bocco, Okwi, Shiza Kichuya na wengine waliopewa mapumziko marefu, wataungana na wenzao.
Kocha wa timu hiyo, Masoud Djuma alisema ; “Wachezaji wetu wale ambao walikuwa kwenye mapumziko wataungana na wenzako mara baada ya michuano ya Kagame kumalizika sababu michuano ikimalizika watapewa mapumziko kama siku nne hivi baada ya hapo ndipo wote wataweza kuungana na kuanza maandalizi.”
Simba ilitumia kikosi tofauti katika michuano ya SportPesa Super Cup na kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Gor Mahia kwa kufungwa mabao 2-0.
Lakini ikapoteza tena katika fainali ya Kombe la Kagame, ikilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Azam FC. Ikiwatumia Meddie Kagere ‘Medi Magoli’, Marcel Kaheza, Mohammed Rashid.
Yale makali yao waliyoonyesha kwenye Kagame na kuwafurahisha mashabiki wa Msimbazi achana nayo, sahau kabisa.
Sasa goma linaanza upya, yaani ndio kwanza kumepambazuka.
Wenye timu yao ambao ni Shiza Kichuya, Emmanuel Okwi na John Bocco wanajiunga na wenzao wiki ijayo tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu.
Simba iliwapa mapumziko baadhi ya nyota wake wakiwemo Okwi na Bocco pamoja na Haruna Niyonzima, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Kichuya na Shomari Kapombe baada ya kuwatumia kwenye michuano ya SportPesa isipokuwa Okwi na Bocco
0 Comments:
Post a Comment