Tuesday 7 August 2018

Simba Day live on Azam Sports 2

Uongozi wa klabu ya Simba kwa kushirikiana na Azam Media wamehakikisha kila Mwana Msimbazi popote alipo hakosi uhondo wa SIMBA DAY hapo kesho.

Kwa wale walio Dar na maeneo ya jirahi hakuna shaka watafurika uwanja wa Taifa kumshuhudia 'Mnyama' akifanya yake dhidi ya Asante Kotoko.

Lakini kwa wale walio mbali na hata nje ya nchi wataweza kuyashuhudia matukio yote ya SIMBA DAY mbashara kupitia runinga zao.

Azam Sport 2 itarusha mchezo wa Simba dhidi ya Asante Kotoko mbashara kuwapa uhondo wale watakoshindwa 'kutimba' uwanja wa Taifa.

Kesho ndio kilele cha SIMBA DAY, Tanzania itasimama kwa masaa kadhaa..!

SIMBA DAY ndio habari ya mjini....!

0 Comments:

Post a Comment