Monday 6 August 2018

Simba to introduce new Jersey today


Uongozi wa klabu ya Simba unatarajia kutambulisha jezi zake mpya leo majira ya saa 5 asubuhi zitazotumika kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Haji Manara, amesema watatmbulisha jezi hizo maalum kwa ligi ambazo zitakuwa za nyumbani na ugenini.

Manara amesema wameamua kufanya maamuzi ya kutambulisha jezi hizo kuelekea Simba Day ili kuwafanya mashabiki na wanachama wa timu hiyo kuzinunua kwa wingi ili waweze kwenda nazo Uwanjani Jumatano ya wiki hii.

Katika tamasha hilo ambalo hufanyika Agsoti 8 kila mwaka, Simba itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana kwa ajili ya kukitambulisha rasmi kikosi chake kipya.

0 Comments:

Post a Comment