Mchezo wa kwanza wa Yanga wa ligi kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliokuwa umepangwa kupigwa August 23 mkoani Morogoro sasa utapigwa uwanja wa Uhuru.
Mapema leo Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imefanya marekebisho ya ratiba mzunguuko wa kwanza.
Aidha baadhi ya michezo ambayo ilikuwa ichezwe kwenye uwanja wa Taifa kati ya August 22 na Septemba mosi imehamishiwa kwenye uwanja wa Uhuru baada ya Serikali kutoa taarifa kuwa itakuwa na matumizi na uwanja huo.
0 Comments:
Post a Comment