Saturday, 19 January 2019

FT: Vita Club 5-0 Simba

Mchezo wa raundi ya pili ligi ya mabingwa barani Afrika kundi D kati ya AS Vital Club dhidi ya Simba umemalizika kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 5-0

Vita ilikuwa bora kwenye mchezo huo kwa kutengeneza nafasi nyingi na ushindi huo wamestahili

Pongezi za kipekee anastahili mlinda lango Aishi Manula kwani aliinusuru Simba isifungwe mabao mengi zaidi

Wachezaji wa Simba walionekana kupooza sana katika mchezo wa leo huku safu ya ulinzi ikionekana kushindwa kumudu mikikimikiki ya washambuliaji wa Vita waliokuwa wakishambulia kwa kasi na nguvu

Matokeo hayo yameishusha Simba hadi nafasi ya tatu huku Vita ikipanda nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao

Al Ahly inaongoza kundi D ikiwa na alama nne, Vita na Simba zote zina alama tatu wakati JS Saoura ina alama moja

Mchezo unaofuata Simba itasafiri kwenda nchini Misri kuikabili Al Ahly, Februari 02 2019

0 Comments:

Post a Comment