Uongozi wa Simba umeshusha wachezaji wawili wa Kimataifa ambapo wameanza majaribio leo kabla ya kufikia makubaliano ya kuwasajili
Wachezaji hao mmoja ni mlinzi wa kati na mwingine ni mshambuliaji, wanaweza kuongezwa kwenye kikosi cha Simba kinachoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa
Simba bado ina nafasi za wachezaji wawili ili kukamilisha idadi ya wachezaji 30
Wachezaji hao mmoja ni raia wa Ghana na mwingine ni raia wa Togo
Baada ya ukosoaji mkubwa katika usajili wa Zana Coulibaly ambaye ameshindwa kuonyesha makali, benchi la ufundi la Simba limeamua kuwafanyia makaribio nyota hao kabla ya kuingia nao makubaliano
0 Comments:
Post a Comment