Friday, 17 March 2023

Abadili Jinsia Na Kuwa wa Kike

Zaya Wade ni Mtoto wa kiume wa mchezaji mstaafu wa Basketball nchini Marekani Dwyne Wade ambaye alizichezea clubs kama Miami Heat, Cleveland Cavaliers na Chicago Bulls.

Huyu Mtoto wa kiume aliamua kubadilishia Jinsia na Kuwa wa kike baada ya kupata ushauri na Support kubwa kutoka kwa mama yake wa kambo Gabrielle Union, baadaye baba yake naye akamuunga mkono.

👉Najua unajiuliza, why mama wa kambo, je mama mzazi yuko wapo?

Mama mzazi wa Zaya anaitwa Siohvaughn Funches ambaye aliachana na Wayne Wade ndiyo maana Mtoto Zaya akalelewa na mama wa kambo.

Baada ya mwanamama Siohvaughn Funches kusikia tetesi Kuwa Mtoto wake wa kiume anataka kubadilisha Jinsia na jina, aliamua kwenda kufungua kesi katika mahakama ya Los Angeles akidai Kuwa huu ni mpango wa Mke mwenzake (Gabrielle Union) na aliyekuwa Mume wake kutaka kupoteza uzao wake.

Pia Siohvaughn alidai Kuwa, mzazi mwenzake anamtumia Mtoto kama kitega uchumi ili apate misaada na udhamini kutoka kwa watu wanaosupport mapenzi ya Jinsia Moja huku akiituhumu direct kampuni ya Disney.

Ila cha kushangaza ni Kuwa Hata mahakama nayo iliamua kumuunga mkono kijana huyu na hatimaye akajibadilisha na Kuwa wa kike akabadilisha na jina kwani kabla hajajiita ZAYA alikuwa anaitwa ZION.

Kwa sasa Zaya ni mwanamitindo ( Model)  nchini Marekani.

👉Unajifunza nini hapa kwenye hii story ya Zaya


0 Comments:

Post a Comment