Straika hatari wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele.
KUELEKEA mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, straika hatari wa Yanga, Mkongomani, Fiston Mayele amechimba mkwara mzito kuwa licha ya kwamba ni mara ya kwanza kwao kucheza hatua hiyo lakini wanaamini wana nafasi kubwa ya kushinda ubingwa huo.
LEO Jumapili Yanga wanatarajiwa kuwa wenyeji wa USM Alger katika mchezo wa fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Mayele kwenye mashindano hayo ndiye kinara wa ufungaji akiwa ameweka kambani mabao sita sawa na mshambuliaji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Ranga Chivaviro.
Nyota huyo ameongeza kuwa hatawaacha wapinzani wake hao kwa kuwa anataka kufunga bao dhidi yao.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mayele alisema: “Tunafahamu huu ni mchezo ugumu kwa kuwa ni fainali na tunacheza dhidi ya timu ngumu na ni mara ya kwanza kwetu kufikia hatua hii kama mchezaji binafsi nina jukumu kubwa la kuisaidia timu kushinda ubingwa huu.
“Tumekamilisha maandalizi yetu na tupo tayari kuhakikisha tunashinda ubingwa, tunajua huu ni mchezo wenye presha kubwa lakini tupo hapa kuipigania nchi kushinda na nitafurahi nikifunga bao.”
0 Comments:
Post a Comment