Michezo ya raundi ya mwisho kwenye mchujo wa Ligi Kuu Ubelgiji wikiendi ijayo ndio iliyobeba matumaini kwa nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta kutwaa ubingwa wake wa pili 'Jupiler Pro' akiwa na KRC Genk.
KRC Genk ipo nafasi ya tatu kwenye mchujo huo wa ubingwa huku wakiwa na pointi 45, wapo nyuma kwa tofauti ya pointi moja tu waliyoachwa na Royale Union Saint-Gilloise (46), Royal Antwerp (46) ambazo zipo kwenye nafasi ya kwanza na pili zimetenganishwa kwa utofauti wa mabao.
Ushindi wa mabao 3-1 ambao chama la Samatta liliupata Jumapili wakiwa ugenini dhidi ya Club Brugge ambao ni mabingwa watetezi, umewafanya kuwa na nafasi kwenye mbio hizo za ubingwa ambazo zitaamuliwa kwenye raundi ya mwisho wikiendi ijayo.
Katika michezo hiyo ya kuamua ubingwa wa wawakilishi wa taifa hilo kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao, KRC Genk itakuwa nyumbani Cegeka Arena kucheza dhidi ya Royal Antwerp ambayo Samatta aliwahi nayo kuichezea kwa mkopo.
Upande mwingine, Saint-Gilloise ambayo ilitoka sare Jumapili ya bao 1-1 dhidi Royal Antwerp itakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Club Brugge.
0 Comments:
Post a Comment