STRAIKA wa Marumo Gallants, Ranga Chivaviro amekataa ofa ya kutoka klabu ya Libya, Al Akhdar akiendelea kuvuta muda kabla ya kuamua wapi pa kwenda.
Chivaviro mwenye umri wa miaka 30 amefuatwa na klabu kibao ikiwamo Yanga, Richards Bay, Sekhukhune United, Future FC na klabu hiyo ya Libya ambayo alikumbana nayo kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Ripoti zinafichua kwamba Al Akhdar ilitenga ofa ya Dola 150,000 kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mmoja zaidi, lakini straika huyo, aliyefunga mabao 17 kwenye michuano yote msimu huu akiwa na kikosi hicho cha Gallants kilichoshuka daraja amewagomea kuendelea na mzungumzo kwa sasa akifikiria juu ya hatima ya maisha yuake ya mpira.
Mwenyekiti wa Gallants alifichua hivi karibuni kwamba wameamua kukifanyia kazi kipengele cha kumwongezea mwaka mmoja mshambuliaji huyo ambacho kilikuwa kwenye mkataba wake, hiyo ina maana Chivaviro hatapatikana bure kwenye dirisha lijalo la usajili mwishoni mwa msimu huu.
Hata hivyo, kipengele hicho kiliwekewa makubaliano kwamba mchezaji anaweza kupinga kuongezewa mwaka mmoja kama timu itashuka daraja. Na sasa wakati maandalizi ya msimu mpya wa 2023/24 yakiwa yamebakiza mwezi mmoja, straika huyo na kambi yake walisema kwamba hakuna haja ya kuharakisha mambo hasa kwa kipindi hiki ambacho Kaizer Chiefs nao wanaripotiwa kuhitaji huduma yake.
0 Comments:
Post a Comment