WAKATI mwingine wa kuendeleza furaha kwa familia ya michezo inakuja siku ambayo Afrika itakuwa ikifuatilia habari za dakika 90.
Ni dakika 90 zenye maamuzi ya dakika 90 za mwisho kwa Yanga kwenye mchezo wa fainali ya kwanza hatua ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Kila mmoja anatambua kazi iliyopo mbele sio ndogo kutokana na ukubwa wa mashindano pamoja na kila timu kuhitaji kutwaa ubingwa.
Yanga haijafika hapo kwa bahati mbaya ipo wazi bali mipango na uthubutu wa wachezejazi kila wakati katika kusaka ushindi.
Tunaamini kwamba ikiwa walipata ushindi kwenye mechi za mtoano na kuonyesha tofauti kwenye kila idara basi muda uliopo kwa sasa ni kuonyesha utofauti kwenyehatua ya fainali.
Mbinu za mchezo wa fainali huwa zinakuwa tofauti lakini bado unabaki kuwa ni mchezo wa mpira ambao unahitaji matokeo kwenye kila mechi.
Kushinda ni jambo la kwanza na kushindwa ni jambo jingie hivyo muhimu kwa kila mmoja kufanya kweli kwenye maadalizi yake.
Wachezaji ni muda wenu kufanya kazi kwa vitendo na kuweka kando masuala yote ambayo hayatakuwa na matokeo kwenye dakika 90.
Makosa yale yasiyo na ulazima ni muhimu kuyaepuka kwa nguvu kubwa kupata ushindi huku umakini ukipaswa kuongezeka.
Kila timu ina nafasi ya kupata matokeo kikubwa ni namna ya kutumia nafasi ambazo zitapatikana na muda ni sasa.
Mashabiki jitokezeni kwa wingi uwanjani kuwashangilia wachezaji hili litaongeza nguvu kimataifa.
0 Comments:
Post a Comment