Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewaita kazini watumishi wa kada ya afya 5,319 wakiwemo wasaidizi wa afya na madaktari kwa ajili ya kutoa huduma katika vituo vya afya mbalimbali kote nchini.
Orodha ya Waombaji ajira iliyochapishwa leo Juni 5, 2023 katika kurasa 357 imehusisha pia wateknolojia, maafisa afya, watoa tiba kwa vitendo, wauguzi na tabibu.
Waziri wa Tamisemi, Angellah Kairuki amesema Waajiriwa wapya ambao hawataripoti katika vituo walivyopangiwa ndani ya siku 14 kuanzia tarehe ya tangazo hili, watakuwa wamepoteza nafasi zao na nafasi hizo zitajazwa na waombaji wengine wenye sifa waliopo kwenye Kanzidata (Database) ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI.
Mwezi Aprili, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan, alitoa kibali cha ajira ya watumishi 21,200 kati yao 13,130 walikuwa wa kada ya Ualimu na 8,070 wa kada za Afya.
Bofya Hapa http://tamisemi.go.tz Kuona Majina Ya Walioitwa Kazini Idara Ya Afya
0 Comments:
Post a Comment