Baadhi ya walimu ambao ni wanachama wa Chama cha walimu Tanzania (CWT) mkoa wa Njombe wamezungumza na vyombo vya habari wakiomba Rais wa Chama hicho Mwl.Leah Ulaya pamoja na katibu Mwl.Japhet Maganga kujitokeza hadharani na kuwaeleza watanzania sababu zilizowafanya kukataa uteuzi wa kuwa wakuu wa wilaya uliofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mwezi January Mwaka huu.
Mjumbe wa kamati tendaji CWT ngazi ya Taifa kutoka mkoa wa Njombe Mwl.Thobias Sanga kwa niaba ya walimu amesema Chama hicho kwa sasa kimekosa mahusiano mazuri na serikali kutokana na changamoto nyingi ikiwemo viongozi wao wa juu kutokubali uteuzi waliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu zisizojulikana na kuleta taharuki kwa walimu.
"Baada ya jambo lile tumekuwa tukipata wakati mgumu kuwaongoza walimu na tukipata maofisi mabalimbali kupata huduma kwa ajili ya walimu tumekuwa tukiulizwa kwanini mnakataa uteuzi wa Rais,tunataka ajitokeze hadharani na aseme nini kilimvutia kukataa uteuzi wa kuwa mkuu wa wilaya na kuamua kuendelea kuongoza walimu jambo la pili awaambie walimu analipwa shilingi ngapi ambazo zimemfanya akatae kazi aliyopewa na Mh Rais"amesema Mwl.Thobias Sanga.
Aidha amesema mambo mengine wanayohoji ni pamoja na kuto kufuata hatua za manunuzi ya tisheti kwa ajili ya walimu kwenye sherehe za mei mosi,Uhamisho wa walimu usiokuwa wa utaratibu pamoja na kugawa vyeo bila kamati tendaji kuhusishwa ipasavyo badala kutetea uovu wa baadhi ya watendaji na kuendelea kusababisha mpasuko ndani ya Chama.
0 Comments:
Post a Comment