Mkutano huo uliotangazwa kwa mujibu wa ibara ya 20 ya Katiba ya Young Africans SC ya Mwaka 2021 utafanyika kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre uliopo Posta jijini Dar es Salaam.
Ajenda za Mkutano huo zitakua:
1. Kufungua Mkutano.
2. Uhakiki wa wajumbe wanaohudhuria mkutano.
3. Kuthibitisha Ajenda.
4. Kuthibitisha kumbukumbu za mkutano uliopita.
5. Yatokanayo na kumbukumbu za mkutano uliopita.
6. Hotuba ya Rais.
7. Kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka Kamati ya Utendaji.
8.Kuthibitisha hesabu za fedha zilizokaguliwa za mwaka uliotangulia, pamoja na kusomewa mapato na matumizi ya Klabu.
9. Kuthibitisha bajeti kwa mwaka unaofata.
10. Kuthibitisha wajumbe wa Baraza la wadhamini.
11. Kufunga Mkutano
0 Comments:
Post a Comment