Tuesday 18 July 2023

Goli Kipa Mpya Wa Simba

Klabu ya Simba SC ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa golikipa, Medjo Simon Loti Omossola raia wa Cameroon kutoka klabu ya Saint-Eloi Lupopo ya DR Congo.

Simon Omossola mwenye umri wa miaka 25 na anajiunga na Simba kama mbadala wa Aishi Salum Manula ambaye ana majeraha ya muda mrefu.

Simba SC imefikia maamuzi hayo baada ya kuachana na usajili wa golikipa Caique da Santos raia wa Brazil ambaye lilikuwa pendekezo la kocha Robartino kutokana na lugha.

Caique da Santos anazungumza Kireno tu lugha ambayo Simba wamehisi itakuwa shida kwenye kuwasiliana na wachezaji wenzake.


0 Comments:

Post a Comment