Thursday 13 July 2023

Tetesi Za Usajili NBC premier League 2023/2024

Klabu ya Yanga Imefikia Makubaliano ya kununua mkataba wa mwaka 1 uliosalia wa winga huyo raia wa DR Congo, Maxi Mpia Nzengeli mwenye umri wa miaka 23 kutoka Maniema FC ya kwao.

Klabu ya Yanga SC imetaganza kukamilisha usajili wa kiungo Mkabaji, Jonas Gerlad Mkude kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na klabu ya Simba SC.

Mlinzi wa Kushoto wa Klabu ya Simba SC, Mohammed Hussein Zimbwe amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea klabu hiyo mkataba ambao utaisha July 2025.

Mlinzi wa kulia, David Kameta ‘Duchu’ amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu kuendelea kusalia katika kikosi cha Simba SC akitokea Mtibwa Sugar alipokuwa kwa mkopo.

Mlinzi wa kulia wa Klabu ya Simba SC, Shomari Salum Kapombe ameongeza mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba SC hadi Julai 2025.

Baada ya kuikosa saini ya Kiungo wa Singida Fountain Gate FC, Kelvin Nashon sasa uongozi wa klabu ya Simba SC umeanza Mazungumzo na kiungo wa Coastal Union, Mtenje Albano.

Klabu ya Kagera Sugar FC ipo kwenye mazungumzo na Gasper Mwaipas akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Mbeya City kumalizika.

Klabu ya Yanga SC imefikia makubaliano ya kumsajili winga, Maxi Mpia Nzengeli mwenye umri wa miaka 23 kutoka klabu ya Maniema Union ya nchni kwao DR Congo kwa mkataba wa miaka miwili.

Klabu ya Young Africans imefikia Makubaliano ya kumsajili Beki wa kati wa timu ya taifa ya Uganda, Gift Fred kwa mkataba wa miaka mitatu kama Mchezaji huru baada ya mkataba wake na SC Villa.

Klabu ya Simba imekamilisha usajili wa Beki, Che Fondoh Malone mwenye umri wa miaka 24 kutoka Coton Sport FC ya kwao Cameroon.

Klabu ya Singida Fountain Gate FC imekamilisha usajili wa Beki, Joash Onyango raia wa Kenya kutoka Simba SC.

Onyango mwenye umri wa miaka 30 amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Singida Fountain Gate FC hadi July 2026.

Klabu ya Simba SC, imetangaza kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Aubin Kramo Kouamé kutoka Asec Mimosas ya kwao Ivory Coast.

Klabu ya Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa winga, Leandre Willy Essomba Onana raia wa Cameroon mwenye umri wa miaka 23 kutoka Rayon Spots ya Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili.

0 Comments:

Post a Comment