Sunday 16 June 2024

Tetesi Za Usajili Tanzania


- Klabu ya Yanga SC imepanga kuachana na Wachezaji wao Kennedy Musonda na Augustine Okrah kuelekea msimu ujao.

- Nizar Khalfan amesaini mkataba wa kuwa Kocha Msaidizi wa Mecky Maxime katika klabu ya Dodoma Jiji

- Stephen Aziz Ki amekubali kusaini mkataba mpya ndani
ya klabu ya Yanga SC.

- Klabu ya Simba SC iko katika hatua za mwisho kumsainisha mkataba Mchezaji Kelvin Kapumbu (28), Raia wa Zambia anayecheza klabu ya Zesco United. Huu utakuwa usajili wa pili baada ya Joshua Mutale unaosimamiwa na Crescentius Magori aliyekwenda nchini Zambia kuwanasa Wachezaji hao.

- Golkipa wa klabu ya Yanga SC, Djigui Diara amedai kuongezewa mshahara kwenye mkataba wake wa sasa na Viongozi wamekubali.

- Mchezaji wa klabu ya Yanga SC , Zawadi Mauya ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

- Baada ya dili la Joshua Mutale kwenda vizuri kwa klabu ya Simba SC (karibia kukamilika ✅), sasa Simba SC wanahitaji saini ya Mchezaji wa klabu ya Madeama 🇬🇭, Derrick Fordjour (21) ambapo Mchezaji huyo bado anao mkataba wa mwaka mmoja na nusu na waajiri wake Madeama. Kwa mujibu wa Transfermarkt Fordjour anathamani ya dola (125) ambazo ni takribani Shilingi milioni (350,866,031) za kitanzania.

- Taarifa za ndani kabisa zinadai kuwa Rais wa heshima wa klabu ya Simba SC, Mohamed Dewji amemwalika Golkipa wa klabu hiyo Ayoub Lakred nyumbani kwake huko Mjini Dubai ili kumaliza michakato ya kuongeza mkataba ambapo mkataba wa Mchezaji huyo unamalizika Juni 30 mwaka huu na kumekuwa na mazungumzo baina ya Golkipa huyo na klabu ya Simba SC ambayo hayajafikiwa mwafaka na inaelezwa kuwa Lakred anataka dau la Shilingi million 500 ili asaini kandarasi mpya.

 - Klabu ya Yanga SC imekamilisha usajili wa Beki wa kushoto wa FC Lupopo, Chadrac Boka (24), ni Mbadala wa Lomalisa Mutambala ambaye ataondoka mwisho wa huu msimu, huyu Beki huko DR Congo wanamuita Rais wa Maji au Marcelo wa DR Congo.

- Kuelekea msimu ujao klabu ya Mashujaa wameonesha nia ya kuhitaji saini ya Mchezaji wa klabu Yanga SC, Denis Nkane ambae wanaona anaweza kwenda kuwa nyongeza nzuri kwenye kikosi chao

- Klabu ya Simba SC Iko katika mazungumzo na Kiungo Mshambuliaji Sou D'Avila kutoka katika klabu ya LYS Sassandra ya Ligi Kuu Nchini Côté d'Ivoire ili aje kuwatumikia msimu ujao.

- klabu ya Amani Queens imeaga rasmi katika Mkoa wa Lindi baada ya kuibamiza Baobab Queens na kuishusha daraja huku ikielezwa kuwa klabu hiyo imeuzwa Kwa Jeshi la Wananchi (JWTZ) linalomiliki klabu ya Mashujaa FC ya Mkoani Kigoma. Klabu hiyo kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara itatambulika kama Mashujaa Queens na itatumia Uwanja wa Lake Tanganyika Mkoani Kigoma ambapo itakuwa makao yao mapya.

- Kiungo Mkabaji Yusufu Kagoma amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba SC akitokea Singida Fountain Gate FC.

- "Pesa za usajiri niko tayari kutoa mwenyewe kwa kushirikiana na wanachama na wapenzi wa Simba, kwa sasa natafuta Mkurugenzi wa ufundi ambaye atakuwa na jukumu la kusimamia mtandao wa usajili na upembuzi wa kina kabla ya mchezaji kusajiliwa.” - Mangungu Murtaza 

- Philippe Kinzumbi amesajiliwa kama Mchezaji mpya wa klabu ya Raja Club kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya TP Mazembe ya Nchini DR Congo 🇨🇩. klabu ya Yanga SC imemkosa Winga huyo baada ya kushindwana na klabu yake ya TP Mazembe.

- Metacha Mnata amejiunga na klabu ya Singida Black stars zamani ilifahamika Kama Ihefu FC akitokea klabu ya Yanga SC 

- Mchezaji wa klabu ya Simba SC, Henock inonga Baka (30) amejiunga na AS FAR RABATI anayofundisha Nasrdine Nabi kwa mkataba wa miaka miwili. Inonga alisaini mkataba huo kipindi DR Congo 🇨🇩 wakiwa Morocco kujiandaa na michuano ya kufuzu Kombe la Dunia.

0 Comments:

Post a Comment