-Golikipa klabu ya Simba sc Ayoub Lakred amejiunga na FUS Rabat kwa mkataba wa miaka miwili
Kipa huyo kutoka Morocco ameondoka rasmi Simba SC, na amerejea nyumbani kwao Mkataba wake umesainiwa rasmi leo asubuhi.
Golikipa, Aishi Manula anarejea Azam FC baada ya miaka Nane.
Manula ambaye ni kipa Bora wa Ligi Kuu mara SITA, anarejea Chamazi baada ya kudumu Simba SC kwa miaka NANE.
Kila kitu kimeshakamilika ni suala la muda tu kutangazwa kwenye viunga vya Azam Complex.
Katika kile kinachoonekana ni kujiimarisha kwenye Eneo la kiungo wa Ulinzi wekundu wa msimbazi Simba hivi sasa wanahusishwa na kiungo wa Kimataifa wa Niger🇳🇪 ambaye mkataba wake na TP Mazembe🇨🇩 umemalizika msimu huu naye si mwingine Bali ni Oussein Somailla Badamassi kiungo mkabaji kuja kuchukua nafasi ya Fabrice ngoma ambaye Jana amewaaga wanasimba na anatajwa kutimkia Morocco.
Kiungo huyo mwenye miaka 28 amekataa kuongeza mkataba na Tp mazembe kwahiyo kwa sasa ni mchezaji huru .
Mkataba wa Morice Chukwu (22) na Singida Black Stars unamalizika mwishoni mwa msimu huu na tayari mazungumzo ya mkataba mpya yamefanyika
- Hatua za kusaini mkataba mpya zipo ukingoni, na hakuna wasiwasi ni kuwa ataendelea kucheza Tanzania
Klabu ya Young Africans inaelekea kukamilisha usajili wa kiungo mkabaji wa Klabu ya Mlandege fc Abdulnasir Mohamed Abdallah (Casemiro)
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 ni moja ya wachezaji vijana walionesha viwango bora katika Ligi Kuu ya Zanzibar na kuisadia timu yake kubeba ubingwa wa ligi hiyo.
Klabu ya Young Africans inatazamia kusajili Nyota hawa msimu huu wa Joto;
•IBRAHIM KEITA - Wing back kutoka TP MAZEMBE✅
•ARTHUR BADA - Kiungo Mshambuliaji kutoka Singida BS✅
•FEISAL SALUM - Kiungo Mshambuliaji kutoka Azam✅ Ambaye pia anawaniwa na Timu ya SIMBA SC
Klabu ya Simba Sc nayo haiko mbali katika maboresho ya kikosi chake ikiwa inawatazamia wafuatao hawa ambapo kocha Fadlu Davis anasema ikiwa wachezaji hawa watasajiliwa pataongezeka Kiungo mmoja tu kikosi chake kikamilike
•FEISAL SALUM - Kiungo Mshambuliaji
•CELESTIN ECUA - Mshambuliaji kinara kutoka ASEC MIMOSAS
WANAOTAZAMIWA KUUZWA MSIMU UJAO
•ELLIE MPANZU >>KRC GENK inayoshiriki Ligi kuu Ubeligiji
•JEAN AHOUA >>Kaizer Chiefs inayoshiriki ligi kuu Afrika Kusini
•CLEMENT MZIZE >> ZAMALEK inayoshiriki Ligi kuu Misri
Tetesi kutokea Simba SC zinaeleza kuwa uongozi wa timu hiyo hauna mpango wa kumuuza kiungo wao Augustine Okejepha raia wa Nigeria Kwa kuwa Wana mpango nae wa muda mrefu.
Orlando Pirates ya Afrika Kusini inatajwa kuiwinda saini ya Mnigeria huyo ambae amejiunga na Simba SC kipindi Cha dirisha kubwa la usajili mwaka huu.
Kwa sasa, hakuna taarifa rasmi au tetesi zinazothibitishwa kuhusu klabu ya Simba SC kuwa katika harakati za kumsajili Jean Claude Girumugisha, mchezaji wa Al Hilal Omdurman ya Sudan. Jina lake halijatajwa katika orodha ya wachezaji wanaohusishwa na Simba SC kwa msimu wa 2024/2025.
Klabu ya Yanga imefungua rasmi mazungumzo na mchezaji wa Azam Gibril Sillah, raia wa Gambia miaka 26, ambaye mkataba wake na wana lambalamba unaisha mwisho wa msimu huu.
Kwa taratibu za usajili Sillah anaruhusiwa kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa kuwa mkataba wake hauzidi miezi sita.
Azam imejaribu kumwongezea mkataba lakini mazungumzo yao hayajafikia mwafaka huku Sillah akihitaji changamoto mpya, hivyo Yanga inataka kumsajili dirisha kubwa la usajili kuimsrisha kikosi chake.
Mchezaji wa Kimataifa wa Gambia, Gibril Sillah 🇬🇲 ameaga rasmi ndani ya kikosi cha Azam FC kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram. Kuelekea msimu wa 2025/26 Sillah hatokuwa sehemu ya kikosi cha wanalambalamba!🍦
0 Comments:
Post a Comment