













Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imefuzu hatua ya robo fainali ya CHAN baada ya kushinda mechi tatu mfululizo na kujikusanyia alama tisa.
Tanzania iliifunga Burkina Faso 2-0, ikashinda 1-0 dhidi ya Mauritania na imeibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Madagascar ambapo ushindi huu umeihakikishia nafasi ya kuendelea hata kabla ya mchezo wa mwisho dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Kutokana na ushindi huo kama Stars itapoteza mechi hiyo ya mwisho tayari imejihakikishia nafasi ya kusonga mbele, ni mafanikio makubwa kwa kikosi hicho ambacho kimeonesha uwezo mkubwa na nidhamu ya hali ya juu katika mashindano haya.
0 Comments:
Post a Comment