Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele, amewakabidhi fomu za uteuzi Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, na Mgombea Mwenza wake, Fatma Abdulhabib Ferej.
Hafla hiyo imefanyika leo, Septemba 13, 2025, jijini Dar es Salaam, mara baada ya wagombea hao kupitishwa rasmi na Tume kuwania nafasi za Urais na Makamu wa Rais katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Katika tukio hilo, Mpina aliambatana na viongozi waandamizi wa chama hicho pamoja na wafuasi waliokuwa wakishangilia hatua ya chama chao kufanikisha uteuzi huo.
Kwa mujibu wa INEC, hatua ya leo inathibitisha kuwa ACT-Wazalendo sasa ni miongoni mwa vyama vilivyokamilisha rasmi mchakato wa uteuzi wa wagombea wa nafasi ya juu ya uongozi wa taifa.
Wachambuzi wa siasa wanasema hatua hiyo inaashiria kuanza rasmi kwa kinyang’anyiro cha urais, ambacho mwaka huu kimeelezwa kuwa na ushindani mkali kutokana na idadi ya wagombea na mikakati yao ya kampeni.
0 Comments:
Post a Comment