Wednesday 18 July 2018

Afariki dunia akiongeza ukubwa wa makalio

Daktari wa ubadilishaji viungo anayefahamika kwa jina la Dokta Bumbum ametoroka baada ya kusababisha kifo cha mwanamke mmoja aliyemchoma sindano kwa ajili ya kukuza makalio.

Wapelelezi wanasema dokta Denis Furtado alifanya kitendo hicho kwa Lilian Calixto katika makazi ya daktari huyi Rio de Janeiro, lakini aliungua wakati wa mchakato huo.

Dokta Furtado alimpeleka hospitali ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na akapoteza maisha, saa kadhaa baadae, Polisi alieleza.

Dokta Denis Furtado ana takriban wafuasi 650,000 kwenye ukurasa wa Instagram

Kisha alitoweka na Jaji ametoa waranti ya kuwezesha kukamatwa.

Dokta Furtado alionekana kwenye Televisheni ya nchini Brazil na ana wafuasi takriban 650,000 kwenye mtandao wake wa Instagram.

Bi Calixto, mwenye miaka 46, mwenye ndoa na watoto wawili akifanya kazi ya benki, alisafiri kutoka mji wa Cuiaba, katikati ya Brazil kwa ajili ya kwenda kuuza makalio siku ya Jumamosi.Ripoti zimeeleza.

Zoezi hilo lililohusiaha pia kuchoma sindano lilifanyika nyumbani kwa daktari.

Lilian Calixto alisafiri mpaka kwa daktari Furtado kwa ajili ya kukuza makalio

Hospitali ya Barra D'Or mjini Rio de Janeiro imesema, ingawa kulifanyika jitihada za kumuokoa Calixto, jitihada hizo hazikuzaa matunda na akapoteza maisha asubuhi ya Jumapili.Sababu ya kifo chake haijathibitishwa.

Polisi wanasema mpenzi wa dokta Furtado amekamatwa akishukiwa kushiriki tukio hilo.

Baraza la kitabibu mjini humo (Cremerj) limesema limefungua jalada la upelelezi kufahamu chanzo cha kifo cha mwanamama huyo.

Rais wa jumuia ya madaktari wa upasuaji viungo Niveo Steffen amesema kuna wimbi kubwa la madaktari wasio wataalamu katika sekta ya afya.

''Huwezi kufanya kazi hiyo ukiwa nyumbani kwako'' , aliliambia shirika la habari la Ufaransa, AFP.

Mwanamke afariki kufuatia upasuaji wa kuongeza maziwa yake ukubwa Kenya

Wasichana wadogo Uingereza wafanyiwa upasuaji uke wao

''Watu wengi wanapatiwa huduma kinyume na ueledi, na watu wanavutiwa kwa sababu ya gharama ndogo, bila kujali kuwa afya zao ni muhimu zaidi

Daktari huyo amewavutia wengi akiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Mbali na kuwa Instagram ana anuani kwenye mtandao wa Facebook ukurasa wake akiwa ameujaza kwa picha zinazoonyesha makalio ya wanawake kabla na baaa ya upasuaji.Huku kwenye Youtube akitoa ushauri kuhusu mpangilio wa chakula na maradhi yanayohusiana na uzazi.

Daktari huyo alieleza mtandaoni kuwa jina la dokta Bumbum alipewa na wateja wake akionyesha kuvutiwa nalo.Jina ambalo amekuwa akilitumia mtandaoni akitoa mafunzo.

0 Comments:

Post a Comment