Thursday 19 July 2018

Kelvin Yondan aigawa Yanga

HUKU tetesi zikizidi kuzagaa kuwa ameshakubali kujiunga na Simba, uongozi wa klabu ya Yanga umevurugwa na taarifa hizo wakati huu ukihaha kumbakisha Kelvin Yondani. 

Mpaka sasa Yondani hajasaini mkataba mpya na klabu hiyo huku kukiwa na tetesi kuwa ameshamaliza biashara na Simba ingawa yeye mwenyewe hakuwa tayari kuthibitisha hilo. 

Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Usajili ya timu hiyo, ambaye hakuwa tayari kutajwa jina lake, alisema bado hakuna muafaka uliopatikana na Yondani. 

"Bado tunaendelea na mazungumzo naye...lakini hatuna uhakika sana kwa sababu hajafanya maamuzi," alisema mjumbe huyo. 

Yondani hakusafiri na timu hiyo kwenda Kenya kwenye mechi ya jana usiku dhidi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gor Mahia. 

Hata hivyo, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma jana alipoulizwa kama wapo kwenye mchakato wa kumsajili beki huyo aligoma kuzungumzia. 

"Hilo la Yondani siwezi kulizungumzia..., sina cha kuongea kwa sasa tunajiandaa na safari ya Uturuki kuweka kambi," alisema Djuma. 

Mkataba wa Yondani na Yanga umemalizika mwezi uliopita na bado hajasaini mpya sambamba na beki wa pembeni Hassan Kessy ambaye naye hakusafiri na timu.

0 Comments:

Post a Comment