Saturday 21 July 2018

Bodi ya Ligi imefafanua wachezaji wa kigeni wanaotakiwa kusajiliwa

Jana Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura alifafanua aina ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kusajiliwa na timu zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.

Hivi karibuni TFF iliongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka saba hadi 10 huku ikiruhusu wachezaji wote kuweza kutumika katika mchezo mmoja.

Wambura amezitaka timu zinazosajili wachezaji wa kigeni kuhakikisha wachezaji hao wana ubora wa kutosha na si ilimradi awe anatoka nje ya Tanzania.

Wambura pia amesisitiza vilabu kuwa na uhakika wa kuwalipa wachezaji hao stahiki zao kwa wakati. 

Timu zitakazosajili wachezaji wa kigeni halafu zikashindwa kuwalipa zitachukuliwa hatua.

Uamuzi huo wa kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni unaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili kwa Afrika baada ya DR Congo kuruhusu idadi kubwa ya wachezaji hao.

DR Congo haijaweka ukomo wa idadi ya wachezaji wa kigeni wanaoweza kusajiliwa na timu zinazoshiriki ligi nchini humo.

0 Comments:

Post a Comment