Saturday 21 July 2018

Kiungo mpya ni miongoni mwa wachezaji waliokwenda Uturuki

Kiungo Mzambia Chama Clotous ni miongoni mwa wachezaji wa kikosi cha Simba waliofanyiwa vipimo vya afya jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili tayari kwa safari ya Uturuki usiku wa kuamkia Jumapili.

Clotous aliyetoka klabu ya Lusaka Dynamos inayoshiriki ligi kuu ya Zambia, alitua nchini jana alfajiri tayari kujiunga na mabingwa hao wa Tanzania Bara msimu uliopita.

Clotous pia amewahi kuitumikia ZESCO FC kwa misimu mitatu.

Kikosi cha Simba kinaondoka nchini leo usiku kuelekea Uturuki kuweka kambi ya siku 15 wakitarajiwa kurejea August 05 siku tatu kabla ya SIMBA DAY.

Tayari ratiba ya ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2018/19 imetoka ambapo Simba itashuka kwenye uwanja wa Taifa August 22 kucheza na Tanzania Prisons.

Kabla ya mchezo huo, August 18 Simba itachuana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa dimba la CCM Kirumba Mwanza.

0 Comments:

Post a Comment