Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) itakaa wiki ijayo kujadili hatma ya uchaguzi wa viongozi wapya Simba.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Revocatus Kuuli, amesema kikao hicho kitafanyika wiki ijayo.
Kwa mujibu wa Katiba ya Simba ya mwaka 2014, viongozi wa Simba sasa wanamaliza muda wao mwezi ujao hivyo uchaguzi ulipaswa kufanyika.
Hata hivyo ikumbukwe mwaka huu Simba imeifanyia marekebisho Katiba yake ili kuruhusu mfumo mpya wa uendeshaji.
Katiba hiyo bado iko kwa msajili.
Viongozi wa Simba walituma barua TFF wakiomba mchakato wa kusajili katiba yao ukamilike ndipo wafanye uchaguzi.
Katiba ya Simba iliyopo kwa msajili hivi sasa inamtaka mgombea atakayewania kiti cha Urasi awe na Shahada tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa inaruhusiwa hata ukiwa na cheti cha kidato cha nne.
0 Comments:
Post a Comment