Thursday, 12 July 2018

Kotei akanusha kuomba kuachwa Simba

Kiungo Mghana James Kotei amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa ameomba avunjiwe mkataba wake na klabu ya Simba.

Kotei ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Simba, amesema taarifa hizo sio za kweli.

Kotei anadaiwa kuomba kuondoka Simba baada ya kukosa uhakika wa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza.

Lakini mwenyewe amekanusha na kusisitiza kuwa ataendelea kubaki Msimbazi.

Amesema yeye ni mpambanaji, anajiamini na hawezi kukimbia changamoto. Anaamini atamshawishi kocha wa Simba ili aweze kumpa nafasi.

Ujio wa kiungo Fabrice Mugheni kutoka Kiyovu Sports umemuweka hatarini Kotei ambaye msimu uliopita alitumika zaidi kama mlinzi wa kati baada ya kunyang'anywa namba na Jonas Mkude.

0 Comments:

Post a Comment