Monday 16 July 2018

Kikosi cha Simba kuanza mazoezi leo

Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuanza mazoezi leo kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa itakayoanza mwezi Novemba.

Baada ya kukamilika kwa kombe la Kagame, Kaimu Kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma aliwapa wachezaji mapumziko ya siku nne kabla ya kurejea kuanza maandalizi hayo.

Wachezaji wote, walioshiriki na waliokosa michuano ya Kagame wanatarajiwa kuanza mazoezi pamoja kwenye uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam.

Mwishoni mwa wiki hii kikosi cha Simba kinatarajiwa kwenda nchini Uturuki kuweka kambi ya siku 18.

0 Comments:

Post a Comment