Saturday 21 July 2018

Kiungo Mzambia asaini miaka miwili Simba

Kiungo mshambuliaji Clateous Chama aliyetokea klabu ya Dyanamo inayoshiriki ligi kuu ya Zambia amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Simba.

Chama alitua nchini juzi Alfajiri ambapo jana alifanyiwa vipimo vya afya sambamba na wachezaji wengine wa Simba waliokuwa wakijiandaa na safari ya Uturuki.

Kiungo huyo amesaini mkataba Jumamosi jioni masaa machache kabla kikosi cha Simba hakijapaa kwenda Uturuki.

0 Comments:

Post a Comment