Saturday 21 July 2018

Wachezaji wa Simba walivyopokea semina kabla ya kwenda Uturuki

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba kinatarajiwa kuondoka usiku wa leo Jumamosi kuelekea nchini Uturuki kuweka kambi ya siku 15.

Wachezaji 35, benchi la ufundi na baadhi ya viongozi wako kwenye msafara huo unaokwenda Uturuki kuijenga Simba imara.

Kabla ya safari hiyo, kikosi cha Simba kilikutanishwa na wadau wa klabu hiyo ili kupewa Semina maalum.

Kocha Mkuu Patrick Aussems, Abdallah Kibaden, Antony Luvanda, Prof. Mohammed Janabi na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Muungano na Mazingira Mh January Makamba ni miongoni mwa waliopata nafasi ya kuwapa nasaha wachezaji.

0 Comments:

Post a Comment