Thursday 19 July 2018

Kocha Yanga afunguka kilichowaponza kombe la shirikisho


Kikosi cha Yanga kimerejea leo kutoka nchini Kenya ambako jana kililala kwa mabao 4-0 dhidi ya Gor Mahia kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera amesema baadhi ya wachezaji walishindwa kufanya vizuri kwa kuwa hawakufanya mazoezi ya kutosha.

Zahera amesema kuna wachezaji walifanya mazoezi kwa siku nne tu huku wakiwa wametoka mapumziko kwa zaidi ya miezi mitatu.

"Kuna wachezaji wamefanya mazoezi kwa siku nne. Kati yao wengine walikosa michezo ya mwisho ya msimu uliopita hivyo wamekaa nje bila kucheza kwa zaidi ya miezi mitatu"

"Lakini imebidi tusafiri nao hivyo hivyo kwa kuwa hatukuwa na namna"

"Katika hali hiyo tusingeweza kufanya muujiza," amesema Zahera.

Yanga inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa mzunguuko wa nne dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa wiki ijayo, Julai 29 2018.

0 Comments:

Post a Comment