Wednesday 18 July 2018

Kuanzia msimu ujao timu mwenyeji kuchukua mapato yote ya uwanjani

Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka nchini (TPLB) Boniface Wambura leo anatarajiwa kutangaza ratiba ya ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2018/19.

Tukio hilo awali lilipangwa kufanywa juzi lakini liliahirishwa hivyo litafanyika leo Makao Makuu ya TFF, Karume jijini Dar es salaam.

Wakati huo huo, kuanzia msimu ujao timu mwenyeji zitakuwa zinapewa fedha zote za mapato ya uwanjani tofauti na ilivyokuwa misimu ya nyuma kwa ngazi ya Ligi Kuu Bara.

Kulingana na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, mapendekezo hayo yalitolewa na vilabu vyenyewe.

0 Comments:

Post a Comment