Wednesday 18 July 2018

Pale inapofika mahali umekwamba kusonga mbele suluhisho hili hapa


Pale inapofika mahali unaona umekwama na huoni njia ya kukupeleka mbele, suluhisho hapo kwako usijaribu kutafuta njia ya kurudi nyuma, tafuta njia nyingine ya mafanikio itakayokuwezesha kufanikiwa. 

Inapofika mahali pia unaona umekata tamaa na umekatishwa tamaa karibu na  kila kitu katika dunia hii, usisijaribu kuruhusu kweli kukata tamaa huko, tambua ipo njia nyingine ya kukusaidia tena kufanikiwa kwako. 

Ikiwa kuna mtu amekuumiza na unajisikia kulipa kisasi, pia nikwambie hilo sio suluhisho sahihi, unatakiwa kujua jinsi ya kukabiliana na hali hiyo lakini si kulipa kisasi kama ambavyo unataka ufanye, unatakiwa kutafuta njia nyingine nzuri ya kulipa kisasi. 

Inapofika wakati na ukaona kabisa uchaguzi pekee ulionao kwa kile unachotaka kukifanya ni uchaguzi hasi, unatakiwa kuachana na uchaguzi huo mara moja na kufuata chaguzi sahihi yaani uchaguzi chanya utakaokupa matokeo mazuri. 

Kwa kawaida tunakuwa tuna chaguzi nyingi sana mbaya, chaguzi ambazo inafika wakati zinatuangusha wenyewe. Unapaswa kuelewa unashindwa kwenye kitu kimojawapo, chagua njia nyingine ya kukufanikisha. 

Unapaswa kukumbuka, kila unapokuwa katika wakati mgumu, wakati ambao unaona wewe huwezi tena kuendelea mbele, kunakuwa kuna njia nyingine ya kukusaidia kuweza kuendelea mbele, hiyo inaeleweka. 

Watu wengi wanajikuta wanashindwa sana kwenye maisha yao kwa sababu pale wanaposhindwa kuona mafanikio badala ya kutafuta hatua za kuwawezesha kwenda mbele, utakuta wao wanatafuta hatua za kuweza kukimbia. 

Hutakiwi kukimbia changamoto yoyote au kufanya kitu chochote ambacho kinakufanya urudi nyuma. Kila wakati unatakiwa kutafuta njia ya kukuwezesha kuendelea mbele na si kurudi nyuma au kutoroka changamoto. 

Kama kuna watu wanatoroka changamoto zao waache wafanye hivyo lakini isiwe wewe. Amua kabisa wewe kuwa mtu wa kutafuta njia ya mafanikio hata pale ambapo njia hiyo inaonekana kama haipo. 

Kwa kutafuta njia hiyo, milango mingine ya fursa utashangaa unaanza kuiona na kupelekea njia ya mafanikio ionekane kwa uwazi. Hakuna kinachoshindikana kila kitu kinawezekana, ikiwa utaamua kuitafuta njia ya mafanikio yako. 

Fanyia kazi haya na chukua hatua kuhakikisha ndoto zako zinatumia

0 Comments:

Post a Comment