Thursday, 12 July 2018

Simba imejiandaa tayali kuikabili Azam FC

Kikosi cha Simba jana jioni kimeendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Boko Veterans kujiandaa na mchezo wa fainali kombe la Kagame dhidi ya Azam FC utakaopigwa kesho Ijumaa, Julai 13 kwenye uwanja wa Taifa.

Mchezo huo unatarajiwa kuanza saa 10 jioni baada kukamilika kwa mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kati ya Gor Mahia dhidi ya JKU.

Kaimu kocha Mkuu wa Simba Masudi Djuma amesema wamejiandaa kikamilifu kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Simba huenda ikaendelea kumkosa mshambuliaji wake Adam Salamba aliyechanika nyama za paja kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya AS Ports.

Hata hivyo wachezaji wengine wote wakiongozwa na kinara wa mabao Meddie Kagere wako katika hali nzuri, tayari kuibeba Simba kwenye mchezo huo.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mchezo wa kesho utakuwa mgumu kwa kuwa ni mchezo wa fainali utakaohusisha timu zinazofahamiana lakini ana imani kubwa kwa Simba kuibuka na ushindi

0 Comments:

Post a Comment