Thursday, 12 July 2018

Kidao athibitishwa kuwa Katibu Mkuu TFF

Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemthibitisha Kidao Wilfred kuwa Katibu Mkuu wa TFF.

Rais wa TFF Wallace Karia amewaambia waandishi wa Habari katika Mkutano uliofanyika jana Julai 12,2018 Makao Makuu ya TFF Karume, Ilala jijini Dar es salaam.

Kabla ya uthibitisho huo Kidao alikuwa akikaimu nafasi hiyo tangu August 2017.

0 Comments:

Post a Comment