Saturday, 11 August 2018

Namungo FC 0-0 Simba

Mchezo wa kirafiki kati ya Namungo FC dhidi ya Simba umemalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Mchezo huo maalum kwa ajili ya ufunguzi wa uwanja wa Majalimu umepigwa wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi na kushuhudiwa na idadi kubwa ya mashabiki.

Benchi la ufundi la Simba likiongozwa na kocha Mkuu Patrick Aussems lilitumia mchezo huo kuwapa nafasi idadi kubwa ya wachezaji ambao walikosa mchezo dhidi ya Asante Kotoko siku ya SIMBA DAY.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara wanatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam kesho.

0 Comments:

Post a Comment